
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba ameendelea kuona mafanikio ya muziki wake baada ya albamu yake ya Love Sound Different kupakuliwa mara milioni 1 ndani ya siku mbili.
Akizungumza na mwandishi wa safu hii, amesema hiyo ni hatua kubwa sana katika muziki wake, ambapo ni ngumu kufikia katika kiwango hicho kwa siku chache.
Kwa mujibu wa Barnaba tayari albamu hiyo imekuwa ikileta ushindani mkubwa katika albamu bora za Afrika, huku nyimbo zake zikiendelea kufanya vizuri duniani kote.
Amesema albamu hiyo zaidi ya kuwa katika mitandao ya kijamii lakini pia imetoka katika mikoa yote, ambapo amewataka mashabiki kumuunga mkono kwa kununua kwa njia ya kawaida au kupakua kupitia mitandao inayouza kazi hiyo.
“Zaidi ya watu milioni 1 wamepakua albamu yangu kupitia mtandao wa Boomplay ndani ya siku mbili. Nawashukuru sana mashabiki zangu haya ni mapenzi makubwa kwangu,” alisema.