Kwingineko

City yamtaka Paqueta kwa zaidi ya Bil 214/-

KLABU ya Manchester City imetoa ofa ya pauni milioni 70 sawa na shilingi bilioni 214.76 kumsajili kiungo wa West Ham United, Lucas Paqueta, mtandao wa michezo ge.globo wa Brazil umeripoti.

Kwa mujibu wa de.globo, West Ham inasita kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Brazil na inatarajiwa kuhitaji ada zaidi ya pauni milioni 70.

Paqueta alifunga mabao manne katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu England(EPL) na alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kocha David Moyes katika michuano ya Ligi ya Europa Conference baada ya kusaini mwaka uliopita akitokea Lyon kwa ada ya pauni milioni 53.

Man City inataka kuimarisha safu ya kiungo baada ya kuwapoteza Ilkay Gundogan na Riyad Mahrez majira haya ya joto.

Tayari City imemsajili Mateo Kovacic toka Chelsea lakini Kocha Pep Guardiola anataka usajili imara zaidi ili kikosi chake kiwe na uwezo kushindana tena katika nyanja zote msimu huu.

Man City itaanza kutetea taji la EPL ugenini kwenye uwanja wa Turf Moor Agosti 11 dhidi ya Burnley.

Related Articles

Back to top button