Nyumbani

Yanga kuzindua Documentary

KLABU ya Yanga Agosti 7 anatarajiwa kuzindua Documentary ya msimu wa kihistoria 2022/23, Dar es Salaam.

Afisa Habari Yanga Ally Kamwe amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Documentary hii iliyotengenezwa kwa utaalamu mkubwa na yenye hadhi ya kuonyeshwa sinema inakwenda kuwaonyesha wanachama na mashabiki wetu maudhui mengi na makubwa ambayo hauwezi kuyapata sehemu yoyote yaliyoiwezesha Klabu yetu kuwa na msimu wa mafanikio na wa kihistoria”

Kamwe amesema Documentary hiyo ni sehemu ya kwanza kwani Yanga itakuja na mradi mkubwa wa historia ya Klabu toka kuanzishwa kwake, kwa kuandikwa kitabu cha historia ya timu hiyo na kuwashirikisha waandishi nguli nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button