Kwingineko

Zaha ni mali ya Galatasaray

KLABU ya Galatasaray imethibitisha kumsajili winga Wilfred Zaha kwa uhamisho huru.

Zaha mwenye umri wa miaka 30 amekuwa huru baada ya mkataba wake Crystal Palace kufikia mwisho mapema majira haya ya joto na sasa amejiunga na miamba hiyo ya Uturuki kwa mkataba wa miaka mitatu.

Amekuwa akiwaniwa na Saint-Germain, Napoli, Lazio, wapinzani wa Galatasaray, Fenerbahce na vilabu kadhaa vya Saudi Arabia.

Uhamisho wa Zaha kwenda Uturuki umekuja baada ya kufanya vizuri katika miaka tisa aliyocheza Palace akifunga magoli 72 katika michezo 315 ya Ligi Kuu England.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button