EPLKwingineko
Vardy aongeza mmoja Leicester
MSHAMBULIAJI wa Leicester City ‘Mbweha’Jamie Vardy amesaini kuongeza mkataba wa mwaka mmoja utakaomweka kwa Mbweha hao hadi Juni 2024.
Vardy amekuwa kihusishwa kujiunga na Manchester United .
Vardy mwenye umri wa miaka 35 ambaye alijiunga na Mbweha hao kutokea Fleetwood Town mwaka 2012 ni mfungaji wa tatu wa muda wote Leicester akifunga mabao 164 katika michezo 387 mashindano yote.
“Ni wazi niko juu ya mwezi. Mara niliposikia ni kitu ambacho Klabu ilikuwa inaangalia, kulikuwa na jambo moja tu ambalo lingetokea, na nilikuwa naenda kusaini,” Vardy ameaimbia tovuti ya klabu hiyo.
Alikuwa muhimu katika kuiongoza Leicester kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/16 na pia kushinda kombe la FA 2020/21.




