Ligi Daraja La Kwanza
Onana: Siongei sana

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Leandre Onana anakwambia hataki kusema mengi cha msingi mashabiki wasubiri kumuona uwanjani.
Onana amezungumza kwa mara ya kwanza leo akiwa Tanganyika Packers ambako kulikuwa na hafla ya Simba kuingia mkataba wa kibiashara na Benki ya NMB.
“Napenda kuushukuru uongozi wa Simba kwa kunikubali, sitaki kusema mengi lakini nitajitahidi kufanya vizuri ili kuisaidia timu kupata mataji na kufanya timu ijuvunie mimi.” Onana
Simba ilimsajili Onana akitokea Rayon Sport ya nchini Rwanda.



