Ligi Daraja La Kwanza

Simba, Yanga kupigwa Aprili 20

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeupangia tarehe mchezo namba 180 wa Ligi Kuu msimu wa 2023/2024 kati ya Yanga na Simba maarufu kama ‘Kariakoo Derby.

Hatua hiyo ni baada ya klabu hizo kuondolewa kwenye michuano ya CAF Champions League.

“Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba iliyofanyiwa maboresho na kutangazwa February 2024, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa April 20, 2024 kuanzia saa 11:00 jioni”. imeeleza taarifa ya bodi.

Bodi imeeleza tayari Yanga na Simba pamoja na Wadau wengine wa Ligi Kuu wamepatiwa taarifa zote kuhusiana na mchezo huo.

Related Articles

Back to top button