BurudaniMuziki

Diamond atimiza ahadi yake

MSANII wa muziki wa bongo Fleva Nassib Abdul ‘ Diamond Platnums’ ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa muziki baada ya kuachia wimbo mpya mapema leo Julai 4, 2023.

Siku za hivi karibuni msanii huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema kuanzia mwezi Julai mwaka huu atakuwa akiachia ngoma kali bila kituo hadi mwakani.

Msanii huyo ambaye ni mmliki wa Lebo ya muziki ya Wasafi alisema kwakuwa mwezi Julai ni mwezi wa kumbuku ya kuzaliwa kwa Mama yake basi atakuwa akitesa katika soko la muziki hadi mwakani ambapo atampisha msanii mpya anayetarajiwa kutambulishwa kwenye lebo hiyo.

Diamond leo amechia video ya wimbo mpya ujulikanao kama ‘ My Baby’ aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria Chike Ezekpeazu Osebuka ‘Chike’.

Related Articles

Back to top button