BundesligaKwingineko
Bayern yathibitisha kumsajili De Ligt

MABINGWA wa Ujerumani Bayern Munich imethibitisha kumsajili Matthijs de Ligt kwa pauni milioni 68 sawa na shilingi bilioni 186,078,817,600.
Baada ya kuwauza Niklas Sule na David Alaba mwaka uliopita safu ya ulinzi ya Klabu hiyo toka jimbo la Bavaria ilidhoofika lakini kuwasili wa mdachi huyo toka Juventus kunaonekana kutatua tatizo hilo.
De Ligt mwenye umri wa miaka 22 anafikiriwa kuwa mmoja wa mabeki wa kati chipukizi wanaokuja juu barani ulaya.
Hata hivyo ana hatua mpya kuonesha kiwango chini ya kocha wa Bayern Julian Nagelsmann.
De Ligt anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Bayern msimu huu baada ya Sadio Mane, Ryan Gravenberch na Noussair Mazraoui.