Kwingineko

Wachezaji 4 wala umeme mechi mmoja

WACHEZAJI wanne wamepata kadi nyekundi na mchezo kusimama kwa muda kutokana na mvutano uliosababishwa na nyimbo za ubaguzi wa kijinsia wakati wa mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mataifa ya Concacaf kati ya Marekani na Mexico.

Mwamuzi wa mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Allegiant uliopo Las Vegas, Nevada, Marekani alipuliza kipyenga kulimaza mechi dakika 14 kabla ya muda baada ya nyimbo za ubaguzi hizo kuendelea.

Wachezaji wengine nane wamepewa kadi za njano katika mchezo huo na mashabiki kurusha uwanjani vikasha vyenye bia licha ya kuonywa kuwa mchezo ungesimamishwa.

Cesar Montes aliyempiga teke Folarin Balogun wa Marekani pamoja na Gerardo Arteaga wa Mexico wamepewa kadi nyekundu huku Weston McKennie na Sergino Dest wa Marekani nao wakitolewa.

Marekani itacheza fainali ya Ligi ya Mataifa ya Concacaf dhidi ya Canada Juni 19.

Canada imeitoa Panama kwa mabao 2-0 yakifungwa na Jonathan David na Alphonso Davies.

Related Articles

Back to top button