Tetesi

Barca kumsajili, kumtangaza Gundogan

Baada ya kushindwa kumsajili Lionel Messi, Menejimenti ya Barcelona haitaki kumkosa mchezaji mwingine wanayemhitaji zaidi kama Ilkay Gundogan wa Manchester City.

Kwa mujibu gazeti la kila siku la michezo Mundo Deportivo la Hispania mpango wa Barca ni kiungo Gundogan kusaini na kumtangaza baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Juni 10.

Kiungo hiyo wa City ambaye anamaliza mkataba mwisho wa mwezi huu anawaniwa na vilabu kadhaa vikiwemo Barcelona, Borussia Dortmund, Al Ittihad na PSG.

Mkataba wake utakapomalizika City atakuwa huru kwenda klabu anayoitaka na anatarajiwa kuwa mojawapo ya biashara kubwa zaidi za usajili majira ya joto.

Habari zinasema nia ya dhati ya Barcelona kumsajili Mjerumani huyo imeongezeka tangu Messi alipotangaza kuwa hatarudi Camp Nou.

Sasa bodi ya klabu hiyo ya Catalonia inataka kufanikisha usajili wa Gundogan haraka iwezekanavyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button