Ligi Daraja La Kwanza
Matola Kocha Mkuu timu za vijana Simba
KLABU ya Simba imewateua viongozi wapya wawili katika nafazi za kocha na mkuu wa programu za timu za vijana.
Afisa Mtendaji Mkuu(CEO) wa Simba Imani Kajula ametangaza hayo leo Dar es salaam.
“Leo tunatoa taarifa ya kuboresha timu za vijana, ya kwanza ni Mkuu wa Programu za Vijana wa Simba, Patrick Rweyemamu. Hakuna mtu bora kumfanya kuwa Kocha Mkuu wa timu za Vijana kama Selemani Matola. Hii inajumuisha timu za vijana za miaka 20 na miaka 17,” amesema CEO Kajula.
Kajula amesema ukichunguza timu kubwa za Afrika zina timu imara za vijana ambao baadae wanaingia kwenye timu ya wakubwa.




