AfricaAfrika Ya Kati

Hearts of Oak yamsajili Ouatching

KLABU ya Hearts of Oak ‘The Phobians’ ya Accra, Ghana imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Yassan Ouatching.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na The Phobians kwa uhamisho huru akisaini mkataba wa miaka miwili hadi 2024.

Ouatching amekuwa huru tangu Agosti 2021 baada ya kuachana na Klabu ya Mohammeddan inayoshiriki Ligi Kuu ya Bangladesh ambako alitumikia kwa miezi minne tu.

Akiwa Ligi Kuu ya Bangladesh alifunga mabao 3 na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo 12 aliyocheza.

Ouatching amecheza michezo miwili ya timu ya Taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu alipoanza kuichezea timu hiyo Juni Mosi, 2022 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) dhidi ya Angola jijini Luanda.

Related Articles

Back to top button