Muziki

Fetty Wap jela miaka 6

RAPA, Willie Maxwell ‘Fetty Wap’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kukiri shtaka la kupanga njama ya biashara ya madawa ya kulevya ‘Cocaine’ Agosti 2022.

Rapa huyo aliyetamba na ngoma ya “Trap Queen”, alisomewa hukumu hiyo katika mahakama ya shirikisho huko Long Island.

Mkali huyo mzaliwa wa New Jersey na washtakiwa wenzake watano walishtakiwa kwa kula njama ya kumiliki na kusambaza zaidi ya kilo 100 (pauni 220) za heroin, fentanyl na crack cocaine kati ya Juni 2019 na Juni 2020.

Fetty Wap alikamatwa Oktoba 2021 kwa madai ya kushiriki njama ya kusafirisha kiasi kikubwa cha Cocaine, heroini, fentanyl na dawa zingine huko New York City.

Waendesha mashtaka walisema mpango huo ulihusisha kutumia huduma ya Posta ya Marekani na magari yaliyofichwa kuhamisha dawa kutoka Pwani ya Magharibi hadi Long Island, ambako zilihifadhiwa kwa ajili ya kusambazwa kwa wafanyabiashara wa Long Island na New Jersey.

Related Articles

Back to top button