Azam kutwaa mkali wa Al-Hilal

KLABU ya Azam FC, inahusishwa kumsajili mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo ili kuimarisha kikosi chake cha msimu ujao.
Akizungumza na HabariLEO, Kaimu Msemaji wa timu hiyo Hashimu Ibwe, ameeleza kuwa lengo lao ni kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya kufanya vyema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
“Lilepo ni mchezaji mzuri kutokana na takwimu zake msimu huu akiwa na timu yake ya Al Hilal kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa lakini hilo hatuwezi kulizungumzia sababu bado anamkataba na timu yake chamsingi tusubiri msimu utakapo malizika,” amesema Ibwe.
Lilepo anahusishwa na Azam kuziba nafasi ya raia mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Idriss Mbombo ambaye tayari uongozi wa timu hiyo umesema utaachana na mshambuliaji huyo kutokana na kutofikia malengo.
Meneja wa mchezaji huyo amesema wapo tayari kufanya bishsra na timu yoyote ambayo itakuwa tayari kuvunja mkataba na hiyo inatokana na machafuko yaliyopo nchini Sudan ambayo yamesababisha ligi kusimama.
Mwisho.




