EPL
Mac Allister, Martinez waingia rada za Chelsea

CHELSEA wanaweza kuipiku Liverpool katika mbio za kumnunua kiungo wa kati wa Brighton Alexis Mac Allister, 24. (Express)
Chelsea na Manchester United wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 30, huku Tottenham pia wakiwa sokoni kumtafuta mlinda mlango mpya. (Mirror).
Chelsea itamruhusu mlinzi wa Brazil Thiago Silva, 38, kujiunga tena na Fluminense msimu huu wa joto. (Telegraph).




