Europa

BABA: Messi hajasaini kokote

BABA mzazi wa Lionel Messi, Jorge Messi amefunga mjadala unaomhusisha nyota huyo wa PSG kuhamia Al-Hilal “Hakuna tulichokubaliana.”

Katika taarifa aliyoiachia hivi punde Jorge Messi ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyo amesema kuwa “Kiukweli hakuna tulichokubaliana mpaka sasa na timu yoyote, hatutofanya chochote mpaka mwisho wa msimu.”amesema Jorge Messi.

Messi amesema kwa sasa hawezi kuamua chochote juu ya mteja wake mpaka utakapomalizika msimu huu.

“Taarifa zilizopo hazina ukweli ni feki, hazina uthibitisho,” ameongeza baba Messi.

Related Articles

Back to top button