Ligi Daraja La Kwanza
Ligi ya klabu U17 Apr 28
Mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa wachezaji wa klabu wenye umri chini ya miaka 17 msimu wa 2022/2023 utaanza Aprili 28, Dar es Salaam.
Timu zitakazofungua dimba ni Ihefu itakayopambana na Simba wakati JKT Tanzania itakabiliana na KMC.
Timu ya Azam U17 ndio ilikuwa bingwa wa michuano hiyo kwa msimu wa 2021/2022.



