
LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara(SWPL) inaendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa viwanja tofauti.
Yanga Princess itakuwa mwenyeji wa Ceasiaa Queens kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Alliance Girls ni wageni wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa.
Nayo The Tigers Queens itakuwa uwanja wa nyumbani wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuikaribisha JKT Queens inayoongoza ligi hiyo.