EPLKwingineko
Saka mchezaji bora EPL Machi
FOWADI wa Arsenal, Bukayo Saka ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu England(EPL) kwa mwezi Machi huku kocha wake Mikel Arteta akiwachaguliwa kocha bora.

Saka amewashinda wachezaji sita walioorodheshwa kushindania tuzo hiyo wakiwemo Alexander Isak, Alexis MacAllister, Tyrone Mings, Mohamed Salah na mchezaji mwenzake wa Arsenal Leandro Trossard.
Amefunga mabao matatu na kutoa pasi ya mabao mawili iliyofunga Arsenal mwezi Machi.
Kocha Arteta amewashinda Pep Guardiola, Unai Emery na Roberto De Zerbi. Pia alishinda tuzo hiyo Agosti, November, Desemba 2022 na Januari 2023.




