Kwingineko

Messi magoli 800

NYOTA Lionel Messi amefunga goli la 800 wakati timu yake ya taifa ya Argentina ilipoichapa Panama magoli 2-0 wakati wa mchezo kirafiki uliopigwa Argentina.

Fowadi huyo wa Paris Saint-Germain mwenye umri wa miaka 35 amekuwa mchezaji wa pili kufikia idadi hiyo baada ya Cristiano Ronaldo.

Idadi hiyo ya magoli hayo ya Messi inajumuisha 672 katika misimu 17 akiwa Barcelona na 29 aliyofunga akiwa PSG.

Pia ana magoli 99 timu ya taifa, mawili akifunga katika fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022.

Nahodha huyo wa Argentina amefunga goli dhidi ya Panama kwa mkwaju wa adhabu dakika ya 89 kwenye uwanja wa Monumental de Nunez jijini Buenos Aires.

Related Articles

Back to top button