Kwingineko

Kudus awa lulu Ulaya

MANCHESTER United bado ina nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ajax Mohammed Kudus, lakini sasa inakabiliwa na ushindani kutoka klabu kubwa barani Ulaya kupata saini yake.

Habari zinasema Napoli, AC Milan, Inter, Paris Saint-Germain na Bayern Munich zote zimekuwa zikimtazama Kudus, huku timu za Ligi Kuu England Arsenal, Tottenham, Chelsea na Liverpool zote zikituma maskauti Uholanzi kumfuatilia.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 22 hivi karibuni amekuwa katika kiwango bora Ajax akichangia magoli 16 katika mashindano yote.

Awali alicheza Ajax chini ya kocha wa sasa wa Man United Erik ten Hag na mdachi huyo ameweka wazi kwa viongozi wake kuwa Kudus ni mchezaji angependa kufanya naye kazi.

Pia Kudus alikuwa na kiwango cha kuvutia katika timu ya taifa ya Ghana(Black Star) wakati wa michuano ya Kombe la Dunia Qatar 2022 akifunga goli la pili katika ushindi wa Black Stars wa magoli 3-2 dhidi ya Korea Kusini katika hatua ya makundi.

Related Articles

Back to top button