FANyumbani

Azam dimbani ASFC leo

RAUNDI ya tatu ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inaendeleo leo kwa  michezo minne kupigwa viwanja tofauti.

Mchezo unaotarajiwa kuwa kivutio ni kati ya Azam na Dodoma Jiji utakaochezwa uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo mwingine timu za jeshi, Polisi Tanzania na JKT Tanzania zitavaana kwenye uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro wakati Green Warriors itakuwa mwenyeji wa Mbuni kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Nayo Buhaya itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex, uliopo Turiani, Morogoro.

Katika mchezo pekee  wa raundi ya tatu uliopigwa uwanja wa Nyamagana Januari 26, Mapinduzi imeitoa Polisi Katavi kwa mikwaju ya penelti 4-3.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button