BurudaniMuziki

Jux kuitambulisha ‘Sina neno’ nchi nzima

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Juma Mussa ‘Jux’, amepanga kuzunguka nchini nzima kutambulisha wimbo wake mpya wa ‘Sina Neno’ unaofanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio kwa sasa.

Akizungumza na gazeti hili jana,  msanii huyo alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutaka kujiweka karibu na mashabiki wake kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu.

“Ni ziara ya kuutambulisha wimbo wangu mpya, lakini pia kuwashukuru mashabiki wangu ambao wamenipa sapoti kwa muda mrefu tangu nimeingia kwenye tasnia hii ya muziki, lakini pia kwa uvumilivu wao baada ya kimya changu kirefu bila kutoa kazi mpya,” alisema Jux.

Msanii huyo pia alipinga wale wanaosema wimbo huo mpya amemuimbia mpenzi wake wa zamani, Vanessa Mdee ‘V- Money’, akisema hakuna ukweli wowote bali ni ujumbe ambao ulimjia kichwani na kuimba kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wake.

Alisema hana tatizo na mpenzi wake wa zamani na anamtakia maisha mema na familia yake ambayo ameianzisha na hayo ndio matarajio ya kila kijana kuwa na familia.

Alisema baada ya ziara hiyo ana mpango wa kufanya wimbo  na msanii mkubwa kutoka Nigeria na anatarajia kuuachia Desemba au mwanzoni mwa mwaka ujao.

Related Articles

Back to top button