Africa

Waamuzi wa Tanzania kuamua mchezo wa CAFCL

DAR ES SALAAM: WAAMUZI wa Tanzania, Ahmed Arajiga, Hamdan Ally, Ally Ramadhani na Nasir Salum, wameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kati ya Star Sport Academy ya Sierra Leone na RS Berkane ya Morocco.

Mchezo huo utafanyika Oktoba 17, 2026, katika Uwanja wa Samuel Kanyon Doe Sports Complex, uliopo Paynesville, Liberia.

Katika uteuzi mwingine, mkufunzi wa waamuzi, Leslie Liunda, ameteuliwa na CAF kuwa mtathimini wa waamuzi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Merrikh SC ya Sudan na Horoya AC ya Guinea.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Oktoba 24, 2026, katika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda.

Aidha, mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Abdallah, ameteuliwa kuwa kamishna wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya APR FC ya Rwanda na Zamalek SC ya Misri.

Mchezo huo utafanyika Oktoba 16, 2026, katika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda.

Related Articles

Back to top button