Mastaa

Kesi ya Tupac, Keffe D ahukumiwa miaka 40

NEVADA: Duane Davis ‘Keffe D’ rasmi amehukumiwa miaka 40 gerezani kwa kupanga mauaji ya rapa Tupac Shakur ya mwaka 1996.

Kabla ya hukumu hiyo, dada wa Tupac, Sekyiwa Shakur alizungumza kwa hisia mahakamani akieleza maisha na urithi wa kaka yake. Alisema hakuna yeyote katika familia yao aliyebaki vilevile tangu Tupac alipouawa.

Sekyiwa alimfananisha Tupac na viongozi kama Malcolm X, Martin Luther King Jr., John F. Kennedy na wengine, akihoji Dunia ingekuwa wapi kama wangeuawa wakiwa na umri wa miaka 25 kama Tupac. Aliomba jaji ampe adhabu ya juu kabisa.

Mopreme Shakur, kaka wa kambo wa Tupac naye alisema ni jambo la kusikitisha kwamba Tupac hakuwahi kupata watoto wala kushuhudia watoto wa ndugu zake wakikua, na aliomba jaji ampe Keffe adhabu ya juu kabisa.

Waendesha mashtaka walidai kuwa Keffe alinufaika kifedha kutokana na mauaji ya Tupac kupitia kitabu chake na mahojiano mbalimbali, jambo lililosababisha maumivu zaidi kwa familia.

“Huwezi kumchukua mwanaume kutoka kwa familia yake. Huwezi kumnyang’anya uhai wake na mustakabali wake wote, kisha ukaondoka tu kanakwamba hakuna kilichotokea.

“Na hasa pale ambapo mtu huyo ni Tupac Shakur. Dunia haikumsahau yeye wala kifo chake, na vivyo hivyo kwa Las Vegas. Ilichukua miaka 30, lakini sasa, utakabiliwa na mkono wa sheria kwa kitendo chako cha Septemba 7, 1996,” alisema Jaji Carli Kierny.

Aidha, kupitia Mtandao wa The Hollywood Reporter, muda mfupi baada ya kutiwa hatiani, Keffe alisisitiza kuwa hakuwepo kabisa karibu na eneo ambalo Tupac aliuawa na hana hatia.

Ingawa kwa miaka mingi alidai katika mahojiano kuwa alihusika katika kifo cha rapa huyo, mawakili wake wanasena madai hayo yalikuwa ni majigambo tu ya mtu aliyekuwa akijaribu kujinufaisha kutokana na tukio hilo la kutisha la kupigwa risasi.

Keffe anadai siku ya tukio alikuwa kwenye baa moja huko West Los Angeles, karibu na chuo cha UCLA, baada ya pambano la Mike Tyson, mbali kabisa na eneo ambalo Tupac alipigwa risasi na kuuawa kwenye eneo la Las Vegas Strip.

Related Articles

Back to top button