Ligi KuuNyumbani

Mayele mchezaji bora, Mgunda kocha bora Nov

MSHAMBULIAJI wa Yanga Fiston Mayele amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda akichaguliwa kuwa kocha bora.

Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imetoa taarifa hiyo kupitia Idara ya Habari ya Mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB).

Kamati hiyo imesema Mayele amechaguliwa baada ya kuonesha kiwango kizuri Novemba na kutoa mchango mkubwa kwa Yanga ikiwa ni pamoja na kufunga mabao 7 kati ya hayo 3 ya ‘hat trick’ akifunga katika mchezo mmoja.

Mayale ambaye pia alihusika katika upatikanaji wa bao moja kwenye michezo mitano aliyocheza Yanga mwezi huo amewashinda Moses Phiri wa Simba na Saido Ntibazonkiza wa Geita Gold alioingia nao fainali.

Kwa upande wa Mgunda amewashinda Hans Pluijm wa Singida Big Stars na Mecky Maxime wa Kagera Sugar alioingia nao fainali.

Pia kamati hiyo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Liti mkoani Singida Hassan Simba kuwa Meneja Bora wa uwanja Novemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu mindombinu uwanjani.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button