Nyumbani

Yanga yamtambulisha Depu

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji mpya Laurindo Dilson Maria Aurélio maarufu kama Depu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chake katika dirisha dogo la usajili.

Depu amesajiliwa akitokea Ligi ya Poland, hatua inayodhihirisha dhamira ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kuelekea nusu ya pili ya msimu.

Mshambuliaji huyo raia wa Angola anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Yanga katika dirisha hili dogo, akijiunga na Emmanuel Mwanengo, Mohammed Damaro pamoja na Allan Okello ambaye alitambulishwa rasmi juzi.

Ujio wa Depu pia unaambatana na kurejea kufanya kazi na kocha wake wa zamani, Pedro Goncalves, jambo linaloaminika kuwa litamsaidia mchezaji huyo kuzoea haraka falsafa ya timu na mahitaji ya benchi la ufundi.

Yanga imeendelea kuonesha nia ya dhati ya kuboresha kikosi chake ili kuendelea kuwa imara katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa, huku usajili wa Depu ukitarajiwa kuongeza ushindani na ufanisi kwenye safu ya ushambuliaji.

Related Articles

Back to top button