World Cup

Hazard astaafu kucheza timu ya taifa

Kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard amestaafu kucheza timu ya taifa ya nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 31.

Hazard ambaye hucheza nfasi ya kiungo wa kati au winga aliitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Ubelgiji 2008 akiwa na umri wa miaka 17 ambapo amechaza michezo 126 na kufunga mabao 33.

Uamuzi wake umekuja baada ya Ubelgiji kuondolewa Kombe la Dunia katika hatua ya makundi ikipoteza mchezo mmoja, sare mmoja na kushinda mmoja.

Ubelgiji ilikuwa kundi F pamoja na Morocco, Croatia na Canada.

“Ukurasa umebadilika leo. Asanteni kwa furaha yote hii tangu 2008. Nimeamua kustaafu michezo ya timu ya taifa. Nitawakumbuka,” ameandika Hazard kupitia mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button