Nyumbani

Okello: Nina furaha kuwa Mwananchi

DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Allan Okello, amesema ana furaha kubwa kujiunga na klabu hiyo huku akisisitiza kuwa yuko tayari kupigania mafanikio ya timu.

Kupitia ujumbe wake mfupi aliouandika kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kutambulishwa rasmi, Okello alisema:
“Nina furaha kuwa Mwananchi. Daima mbele, nyuma mwiko,” akiambatanisha na alama ya Yanga pamoja na kauli mbiu ya klabu hiyo.

Okello alitambulishwa jana usiku saa tano ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wa Yanga waliokuwa wakisherehekea Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, tukio lililovuta hisia za wanayanga wengi waliomkaribisha kwa shangwe.

Kwa upande wa historia yake, Okello ni mchezaji wa kimataifa wa Uganda aliyewahi kuzichezea klabu za KCCA FC, Paradou AC ya Algeria na Vipers SC, ambako alijijengea jina kwa uwezo wake wa kufunga mabao na kutoa pasi za mwisho.

Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani na ubunifu ndani ya kikosi cha Yanga, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kumuona akianza kuchangia mafanikio ya klabu hiyo.

Related Articles

Back to top button