Muziki

Ambwene Mwasongwe awapa ujumbe wa tumaini mashabiki

DAR ES SALAAM:MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili Tanzania, Ambwene Mwasongwe, amewapa ujumbe wa faraja na matumaini mashabiki wake akisisitiza umuhimu wa kumtegemea Mungu katika kila hatua ya maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ambwene ameandika ujumbe wenye kugusa nyoyo za wengi akisema kuwa bila msaada wa Mungu hakuna binadamu anayeweza kusaidia kwa ukamilifu, lakini Mungu akishasaidia hakuna cha kuogopa wala kushindwa.

“Mungu asipotusaidia hakuna atakayetusaidia. Ila Mungu akitusaidia hakuna wa kututisha wala kutushinda. Nakuombea uzima, afya na amani unapojiandaa kuvuka mwaka huu,” ameandika Ambwene.

Ujumbe huo umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi, huku wakimpongeza kwa kuendelea kutumia jukwaa lake kueneza neno la matumaini, imani na upendo, hasa wakati huu wa mabadiliko ya mwaka.

Related Articles

Back to top button