Muziki

Marioo: Lazima tumalize mwaka kwa kishindo

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Omary Mwanga maarufu kama Marioo, ameahidi kumaliza mwaka kwa kishindo baada ya kufanya vizuri kwenye majukwaa mbalimbali ya kidijitali kwa miaka mfululizo.

Kupitia ukurasa wake, Marioo amesema mafanikio yake yametokana na upendo na sapoti ya mashabiki wake ambao wameendelea kusikiliza kazi zake na kumfanya aongoze kwa muda mrefu kwenye majukwaa ya kusikiliza muziki mtandaoni.

“Upendo na support yenu itaendelea kuishi moyoni mwangu. Asilimia 90 ya digital platforms kwa miaka kadhaa mfululizo nimekuwa naongoza kwa kusikilizwa zaidi.

“Kwa uzito na thamani mnayonipa siwezi kuwaacha hivi hivi. Huu mwaka lazima tumalize kwa kishindo… No Way,” ameandika Marioo.

Msanii huyo, ambaye amekuwa kwenye chati za juu kwa hits mbalimbali, ameendelea kuonyesha kuwa mwaka huu ana mipango mikubwa kwa ajili ya mashabiki wake.

Related Articles

Back to top button