BurudaniMuziki

Sikinde kukata kiu ya mashabiki

MAGWIJI wa dansi nchini, Orchestra Sikinde Original imeapa kukata kiu ya wafia dansi katika siku ya utoaji tuzo za Muziki za Cheza Kidansi  itakayofanyika Dar es Salaam Desemba 9, 2022.

Orchestra Sikinde Original tayari imeibua gumzo kubwa nchini baada ya kutoa vibao vyake vitatu vikali ambavyo ni ‘Mchepuko’, ‘Hila za ndugu’ na ‘sensa’ huku video ya wimbo wa Mchepuko ukitikisa maeneo mbalimbali.

Akizungumza na gazeti la HabariLEO mmoja wa wanawamuziki wa bendi hiyo, Abdallah Hemba alisema pamoja na vibao hivyo ambavyo wameshatoa siku hiyo watatambulisha vibao vingine vikali vipya.

“Lengo letu kila atakayetuona jukwaani siku hiyo awe na tamaa ya kutuona tena siku nyingine sambamba na kutupa mialiko kibao,” alisema Hemba.

“Kwa sasa tuna rekodi tatu tu lakini tunamshukuru Mungu tumeanza kupata mialiko na kupiga shoo kibao kwa wiki maeneo mbalimbali, sasa wakituona tarehe 9 ni matumaini yetu tutaishangaza dunia,” alijigamba Hemba.

Bendi hiyo tayari imejizolea sifa kubwa kutokana na kupiga muziki mtamu hasa nyimbo zilizovuma za bendi mbalimbali mahiri nchini.

Related Articles

Back to top button