Burudani

Sonam Kapoor atangaza ujauzito wa Pili

MUMBAI: MUIGIZAJI na ikoni ya mitindo huko Bollywood, Sonam Kapoor Ahuja, ametangaza rasmi kwamba yeye na mumewe Anand Ahuja wanatarajia mtoto wao wa pili. Wawili hao tayari ni wazazi wa mtoto mmoja anayeitwa Vayu.

Kwa miezi kadhaa mashabiki walikuwa wakihisi kuwa Sonam ana ujauzito baada ya video na picha za uwanja wa ndege kuzua tetesi. Hata hivyo, familia hii maarufu iliamua kusubiri muda muafaka ndipo iufahamishe umma na mashabiki wa msanii huyo kwamba wanatarajia mtoto wa pili
Asubuhi ya leo Alhamisi ya November 20, Sonam alitumia akaunti yake rasmi ya Instagram kutangaza ujauzito wake kwa mtindo wa kipekee na wenye mvuto wa kifahari.

Alichapisha picha kadhaa akiwa amevaa seti ya blazer na sketi ya pinki kali yenye mvuto wa ‘vintage’, moja ya muonekano uliowahi kupendwa sana na Princess Diana.
Katika picha hizo, Sonam alionekana akishika tumbo lake la ujauzito huku akiandika neno moja tu lenye maana kubwa:
“MOTHER .”
Kupitia Instagram Stories, aliendelea kuthibitisha habari hiyo kwa ujumbe mfupi lakini mzito:
“Coming Spring 2026 .”

Mara baada ya tangazo hilo, mumewe Anand Ahuja aliandika katika maoni kwa ujumbe wa upendo na utani. Alimwandikia:
“Baby ma… also chicccccc mama!”
Kwenye ujumbe mwingine akaongeza:
“Double trouble .”

Habari hii imepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake duniani kote, huku wengi wakimpongeza Sonam kwa kutangaza ujauzito wake kwa mtindo na umaridadi na wa kipekee.

Related Articles

Back to top button