Kwingineko

Mbappé kuwakosa Azerbaijan Jumapili

PARIS: SHIRIKISHO la Soka la Ufaransa (FFF) limetangaza Nahodha wa Timu ya taifa hilo, Kylian Mbappé, atakosa mchezo wao wa mwisho wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Azerbaijan Jumapili kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.

“Mbappé bado anasumbuliwa na uvimbe kwenye kifundo cha mguu wa kulia unaohitaji uchunguzi zaidi. Atafanyiwa vipimo leo mjini Madrid,” FFF imesema kwenye taarifa kwa umma.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine siku ya Alhamisi, ushindi uliowahakikishia Les Bleus tiketi ya Kombe la Dunia 2026.

Kiungo wa Manu Koné wa AS Roma na Eduardo Camavinga nao watakosa mchezo huo. Koné atakuwa nje kutokana na kusimamishwa baada ya kuonyeshwa kadi dhidi ya Ukraine, huku kiungo wa Real Madrid ambaye hakushiriki kwenye mchezo wa Alhamisi akipata tatizo la misuli kwenye nyama ya paja la kushoto.

Related Articles

Back to top button