Zuchu atamani ya ndoa

DAR ES SALAAM: MSANII nyota wa Bongo Fleva, Zuhura Othman ‘Zuchu’, ameweka wazi zawadi ya pete ya almasi aliyozawadiwa na mpenzi wake ambaye pia ni staa wa muziki, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Zuchu aliposti picha ya pete hiyo na ujumbe wa shukrani kwa Diamond, akieleza jinsi zawadi hiyo ilivyomgusa na kuomba pete hiyo ndiyo iwe pete yake rasmi ya ndoa, licha ya changamoto wanazopitia kwenye uhusiano wao.
Zuchu ameandika:“To my husband Dplatinum, thank you for bringing me this diamond and gold set. I’m grateful for you. I wanted this ring as my wedding ring. Due to circumstances you didn’t have it then, but you kept.”
Mashabiki wa wawili hao wamekuwa wakijadili ujumbe huo mtandaoni, wengi wakiona ni ishara ya upendo ulioimarika tena kati ya Zuchu na Diamond, ambao mara kadhaa wamekuwa wakihusishwa na misukosuko ya kimahusiano.




