Africa

Baraket: Njooni Azam Complex mle raha

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Azam FC, Baraket Ihmid, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kesho kutwa Ijumaa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kushuhudia historia ikitengenezwa wakati Azam itakapovaana na KMKM ya Zanzibar kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliochezwa Zanzibar, hivyo wanahitaji sare au ushindi wowote ili kufuzu hatua ya makundi.

Baraket amesema mchezo huo ni wa kihistoria kwa klabu hiyo na mashabiki wana nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

“Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi Ijumaa Chamazi. Tunahitaji sapoti yao ili tukamilishe kazi tuliyoianza Zanzibar. Huu ni wakati wa kuandika historia mpya kwa Azam FC,” alisema Baraket.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kocha wa Azam FC, Florent Ibenge, akitarajiwa kuendeleza ubora wa kikosi chake kilichoonesha uimara mkubwa katika michuano hiyo, kwa lengo la kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button