EPL

Goli lililokataliwa na VAR, lawa goli bora la mwezi

LONDON: KLABU ya Fulham imelitangaza Goli lililokataliwa na VAR la Kiungo wa kati wa klabu hiyo Josh King, lililofungwa katika dakika ya 21 ya mchezo dhidi Chelsea wikiendi iliyopita, kuwa goli bora la mwezi Agosti la klabu hiyo

King alikimbia kutoka kwenye eneo lao na kupokea pasi ndefu kutoka kwa Sander Berge na kushambulia lango la Chelsea, alimpindua beki Tosin Adarabioyo wa Chelsea kabla ya kuachia shuti kali la chini chini lililotinga wavuni.

Sherehe za goli hilo la Fulham zilikatishwa ghafla baada ya mapitio ya waamuzi wa VAR kuamua kwamba mshambuliaji wa Fulham Rodrigo Muniz alimkanyaga beki wa Chelsea Trevoh Chalobah katika harakati za kulishambulia lango la Chelsea. Mchezo ulikuwa 0-0 wakati huo, baadae Chelsea walishinda 2-0.

“Goli limepata asilimia 83.1 ya kura zote za mashabiki hii inaonesha umaalum wa tukio lile kwa mashabiki wetu” – Fulham ilisema.

Awali, Mkuu wa bodi ya waamuzi (PGMOL), Howard Webb, alisema uamuzi wa kukataa bao hilo ni kosa na kwamba mwamuzi msaidizi wa video (VAR) alifanya makosa kwa kuingilia kati.

King amekuwa Fulham tangu ajiunge na akademi yao akiwa na umri wa miaka minane, na alicheza mechi yake ya kwanza ya Premier League Desemba mwaka jana. Ameanza mechi zote tatu za ligi za Fulham msimu huu, huku bao hilo huenda lingekuwa lake la kwanza la Premier League.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button