EPL

Ni suala la muda tu Eze kutua spurs

LONDON: TAARIFA kutoka nchini England zinaeleza kuwa klabu ya Tottenham Hotspur imefikia makubaliano na Crystal Palace kwa ajili ya uhamisho wa kudumu wa kiungo mshambuliaji Eberechi Eze msimu huu wa majira ya joto.

Eze amekuwa mmoja wa wachezaji wanaowindwa sana sio tu dirisha hili lakini katika madirisha ya usajili ya siku za karibuni kufuatia mfululizo wa kiwango bora kwa Eagles tangu ajiunge nayo mwaka 2020.

Arsenal waliangalia uwezekano wa kumsajili mapema kwenye dirisha hili, lakini harakati zao zilipungua baada ya Ethan Nwaneri kusaini mkataba mpya na wachezaji waliozidi kikosini.

Tottenham sasa wanaonekana kuwa kinara kwa Mwingereza huyo baada ya kuongeza juhudi katika wiki za hivi karibuni kumnyakua Eze kutoka kwenye kikosi cha Palace wapinzani wao wa London Kaskazini.

Eze aliichezea Palace katika mechi yao ya kwanza ya Premier League dhidi ya Chelsea Jumapili akifunga bao ambalo lilikataliwa kabla ya kuonesha ishara ya kuwashukuru mashabiki wa Palace ishara iliyotafsiriwa kama ya kuaga mwishoni mwa mchezo huo.

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye thamani yake inakadiriwa kufikia pauni milioni 47 anaweza kuwa alicheza mechi yake ya mwisho katika kikosi hicho cha London Kusini, kwani kituo cha ESPN cha England kimesema anaweza kutangazwa muda wowote.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button