Liverpool waanzia walipoishia

LIVERPOOL: Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Liverpool wameanza vyema mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo baada ya kuwatembezea kichapo cha paka mwizi AFC Bournemouth mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa nyumbani kwao Anfield.
Usajili mpya ndani ya kikosi hicho mshambuliaji Hugo Ekitike ndiye aliyeanzisha balaa hilo mnamo dakika ya 37 alipojitengenezea nafasi ambayo aliitumia vyema na kuiandikia Liverpool bao la kwanza.
Kipindi cha pili Liverpool walikuja kwa kasi iliyowashinda Bournemouth na mwenyeji kwenye kikosi Cody Gakpo akitupia chuma ya pili mnamo dakika ya 49. Dakika za jioni Federico Chiesa aliiandikia Liverpool bao la 3 dakika ya 88 baada ya mshambuliaji Antoine Semenyo wa Bournemouth kufanya usomeke 2-2 dakika ya 64 na 76
Mfalme wa Misri Mohammed Salah ndiye aliyemwagia maji mshumaa wa matumaini wa Bournemouth baada ya kufunga bao la ushindi ndani ya dakika 6 zilizoongezwa kukamilisha mchezo huo.
Mchezo huo wa aina yake ulitumika pia kutoa heshima kwa mshambuliaji wao aliyefariki katika ajali ya gari mwezi Juni nchini Hispania Diogo Jota magoli mawili ya Ekitike na Gakpo yakishangiliwa kwa ishara ya namba 20 aliyoivaa enzi za uhai wake.
Sambamba na hilo kulikuwa na tukio maalum mwanzo wa mechi pamoja na mashabiki kusimama na kupiga makofi mnamo dakika ya 20 ya mchezo huo.