Kwingineko

“Modric ni wa kukumbukwa” – Alonso

EAST RUTHERFORD, Maisha ya umashuhuri wa soka ya Luka Modric ndani ya Real Madrid yalitamatika vibaya kwa kuchapwa 4-0 na Paris St Germain katika nusu-fainali ya Kombe la Dunia la Klabu lakini meneja wake na mchezaji mwenzake wa zamani Xabi Alonso amesema urithi wa nyota huyo wa Croatia utakumbukwa na vizazi vingi vya Los Blancos.

Modric mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2018 na mchezaji aliyepambwa zaidi katika klabu hiyo ya Hispania atajiunga na AC Milan baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho akiwa na Real Madrid kwenye Uwanja wa MetLife mjini New Jersey usiku wa Jumatano.

“Huu si mwisho tulioutaka, ni mwisho mchungu, lakini hatakumbukwa kwa mechi ya leo pekee lakini pia mechi nyingine kubwa. Ni gwiji wa soka duniani na Real Madrid. Atakumbukwa kwa mambo mengi mazuri kuliko dakika 25 alizocheza leo.” – amesema Alonso

Tangu kuwasili kwake kutoka Tottenham Hotspur mwaka 2012, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 sasa ameichezea Real Madrid michezo 597 na kushinda mataji 28 yakiwemo mataji sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Related Articles

Back to top button