Kwingineko

Alonso: Tuendelee kumsubiri Mbappe

EAST RUTHERFORD, Kocha mkuu wa Real Madrid, Xabi Alonso amesema ni mapema mno kusema kama mshambuliaji wa klabu hiyo Kylian Mbappe ataanza katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu ya dhidi ya Borussia Dortmund leo usiku fowadi huyo Mfaransa akiendelea kupata nafuu kutokana na ugonjwa wa tumbo.

Mbappe alicheza mechi yake ya kwanza Jumanne wakati Real Madrid ilipoibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Juventus na kutinga robo fainali baada ya kukosa mechi zote za hatua ya makundi.

“Anaendelea kuwa bora. Amekuwa akiimarika katika siku tatu zilizopita, tutatafakari na tutafanya maamuzi ikiwa atakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza dhidi ya Dortmund lakini bado mapema kusema kwa uhakika.”

Mbappe aliingia akitokea benchi kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili cha ushindi wa 1-0 wa timu hiyo ya Uhispania dhidi ya Juventus mjini Miami Jumanne, na kuibua shangwe hali iliyodhihirisha mvuto wake wa kimataifa katika michuano hiyo nchini Marekani.

Kikosi cha Alonso kimekuwa kikimtegemea Gonzalo Garcia kuchukua nafasi ya Mbappe wakati huu hayupo, huku mhitimu huyo wa akademi ya Madrid mwenye miaka 21 akiwa na mabao matatu ikiwa ni pamoja na lile la ushindi wa Jumanne na kusaidia katika matokeo mazuri kwenye mashindano hayo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button