Kwingineko

Miili ya Jota, andre yafikishwa nyumbani

GONDOMAR, Waziri Mkuu wa Ureno Luis Montenegro ameungana na watu wa familia ya Diogo Jota katika hafla ya kuuaga miili hiyo iliyofanyika kwa faragha mapema leo Ijumaa katika mji aliozaliwa mwanasoka huyo wa Liverpool kaskazini mwa Ureno kufuatia kifo chake pamoja na kaka yake Andre Silva katika ajali ya gari nchini Hispania.

Wakala wa muda mrefu wa Jota Jorge Mendes pia alionekana akijiunga na familia hiyo, akiwemo mkewe Rute Cardoso, ambaye alikuwa ameolewa na mwanasoka huyo kwa ndoa ya kanisani wiki chache zilizopita. Montenegro ilitumia karibu nusu saa na familia kabla ya kuondoka bila kutoa neno kwa wanahabari.

Msafara wa magari ya kubebea maiti uliokuwa na miili hiyo ulianza safari ya kuelekea mji wa Gondomar ulio karibu na jiji la Porto jioni ya siku ya Alhamisi kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Puebla de Sanabria, karibu na eneo ambalo gari aina ya Lamborghini ambayo ndugu hao walikuwa wakisafiria lilipata ajali.

Polisi wanasema wanashuku chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya gari hiyo iliyosababisha gari kuacha njia kupinduka kisha kuwaka moto majira ya saa sita usiku.

Ofisi ya meya wa mji wa Gondomar amesema wakazi wa mji huo watapata fursa ya kuaga miili hiyo katika kanisa la Gondomar kuanzia saa 12:00 jioni saa za Afrika Mashariki na mazishi kesho Jumamosi katika kanisa lililo karibu saa ibada ikianza saa 4 asubuhi saa za Hispania.

Related Articles

Back to top button