Mbappe alazwa hospitali Marekani

MIAMI: Klabu ya Real Madrid kupitia tovuti yake rasmi imetangaza kuwa Mshambuliaji wake Kylian Mbappe amelazwa hospitalini nchini Marekani kutokana na maumivu makali ya tumbo mapema leo Alhamisi.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia la 2018 Mbappe alikosa mchezo wa ufunguzi wa Real Madrid kwenye Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya klabu kutoka Saudi Arabia Al Hilal mjini Miami Jumatano kwa sababu ya kile klabu hiyo ilisema ni homa kali.
Kocha wake Xabi Alonso alikuwa na matumaini kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa atakuwepo kwenye mchezo ujao wa timu hiyo dhidi ya Pachuca Jumapili. Lakini kulazwa kwake hospitalini kunatia shaka nia ya kocha huyo mwenye ndoto kubwa Madrid.
“Mchezaji wetu Kylian Mbappé anasumbuliwa na ugonjwa wa tumbo wa ‘gastroenteritis’ na amelazwa hospitalini ili kufanyiwa vipimo kadhaa na kufuata matibabu sahihi,” ilisema taarifa ya Madrid.
Hata hivyo taarifa hiyo haikufafanua kwa kina ni lini mshambuliaji huyo machachari atarejea kukitumikia kikosi cha Los Blancos kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Klabu linaloendelea kwa mud awa mwezi mzima nchini marekani