Muziki

Bebe Cool Atoa Albamu Mpya, ‘Break The Chains’

KAMPALA: MWANAMUZIKI wa Uganda na nguli wa kitamaduni Bebe Cool ametoa rasmi albamu yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya ‘Break The Chains’ yenye maana ya ‘Vunja Minyororo’.

Kwa sasa albamu hiyo inapatikana kwenye majukwaa yote makubwa ya utiririshaji muziki mtandaoni. Albamu hii ina nyimbo nyingi na nyimbo za aina mbalimbali zinazoakisi mageuzi yake.

Akizungumza katika tafrija ya kutoa albamu yake mjini Kampala kabla ya kuachiwa, Bebe Cool amesema, “Huu ni mwanzo wa safari mpya kwa muziki wa Kiafrika na muziki wa Uganda kwa ujumla. Kwa albamu hii, nataka kuhamasisha, kubuni na kuonesha kwamba wasanii wa Afrika wanaweza kufanya biashara ya muziki na kuziuza digital.”

Albamu hiyo in jumla ya nyimbo 17 ina nyimbo za aina mbalimbali zikiwemo za kuburudisha katika taaluma ya Bebe Cool nchini Uganda akiamini kwamba itakuwa utambulisho wa muziki wa Afrika Mashariki, ikijumuisha muziki wa Afrobeats, Afropop, Afrotech na Afro-house.
Albamu ya ‘Break The Chains’ imeshirikisha wasanii mbalimbali akiwemo msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade katika wimbo wa ‘African Love’, nyota anayechipukia wa Uganda, Joshua Baraka katika wimbo wa ‘Cheque’ na DJ wa kimataifa wa Kenya na mtayarishaji DJ Edu amesahirikishwa katika wimbo wa ‘Games’.

Wimbo wa kwanza katika albamu hiyo ‘Circumference’ uliotayarishwa na mkali kutoka Nigeria PhilKeyz, umechanganya midundo ya Afrobeat huku wimbo unaofuata, ‘Motivation’ uliotayarishwa na Bushington na Melanin Boy, wimbo huu unaelezea mapenzi na video ya muziki wake imeongozwa na Garrick Williams kutoka Afrika Kusini.

Safari ya muziki ya Bebe Cool imekuwa ikielezwa tangu siku zake za mwanzo jijini Nairobi kama mmoja wa wasanii wa kwanza kusainiwa na Ogopa Deejays, hadi kufaulu kwake na Necessary Noize kama sehemu ya washindi wa tuzo wa East African Bashment Crew, hajawahi kuacha muziki na ubunifu.

Alitamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo wimbo wa ‘Africa Unite, na ‘Fire Anthem’ na sasa anatoka na albamu mpya mwaka huu 2025 akitangaza muziki wa Afrika kwa ujumla kupitia nyimbo za mapenzi, dansi, na tafakari za kina zinazoangazia masafa ya Bebe Cool na uwezo wa kubadilika.

Related Articles

Back to top button