Kwingineko

Beki Boca juniors akosa Visa ya marekani

Kukosa kombe la Dunia

BUENOS AIRES, Klabu ya Boca Juniors ya Argentina imesema beki wake Ayrton Costa atakosa Kombe la Dunia la Klabu baada ya raia huyo wa Argentina kunyimwa visa ya kuingia Marekani jana Alhamisi.

Costa hakufunga safari kwenda Miami akiwa na wachezaji wenzake Jumapili kwa sababu ombi lake la visa lilikuwa bado likishughulikiwa katika ubalozi wa Marekani mjini Buenos Aires, hata hivyo bado alijumuishwa kwenye orodha ya wachezaji watakaocheza michuano hiyo itakayoanza Jumamosi.

Boca Juniors ilithibitisha kuwa Costa mwenye umri wa miaka 25 alinyimwa visa, lakini haikutoa maelezo kuhusu sababu zilizosababisha sintofahamu hiyo huku duru mbalimbali zikiarifu kuwa Costa alihusika katika kesi ya jinai iliyohusu jaribio la wizi mwaka 2018 mjini Bernal, Argentina.

Kutokuwepo kwake kikosini kunamwacha kocha Miguel Russo bila ya mmoja wa wachezaji wake wanaotarajiwa kuanza kwenye mechi ya kwanza ya Kundi C ya timu hiyo dhidi ya Benfica siku ya Jumatatu huku kundi hilo pia likijumuisha Bayern Munich na Auckland City ya New Zealand.

Sambamba na Costa beki Marco Pellegrino, ambaye alisajiliwa kabla ya Kombe hili la Dunia la klabu, anaendelea kupata nafuu kutokana na maumivu ya misuli. Mkongwe Marcos Rojo anatarajiwa kuanza. Beki huyo alisajiliwa na Boca Juniors Januari iliyopita baada ya muda mfupi akiwa na Royal Antwerp ya Ubelgiji.

Related Articles

Back to top button