Kwingineko

Mastaa watoa neno ajali ya ndege ya India

AHMEDABAD: MASTAA mbalimbali nchini India akiwemo muigizaji filamu, Akshay Kumar wameshtushwa na ajali ya Shirika la ndege India huku kila mmoja akisema lake.

Ndege hiyo ilianguka leo ilianguka leo Juni 12, 2025 muda mfupi baada ya kupaa kutoka Ahmedabad ilikuwa ikielekea katika Uwanja wa ndege wa Gatwick wa London huku ikiwa na abiria 242.

Akshay Kumar katika ukurasa wake wa X ameandika; “Nimeshtushwa na nakosa la kusema katika ajali ya Air India. Ni maombi pekee kwa wakati huu ndiyo yanahitajika” aliandika huku akiwa ameweka picha ikimuoesha akiwa na huzuni kubwa kwa kilichotokea.

Mbali na Akshay, mastaa wengine kadhaa wa Bollywood walioguswa na tukio hilo na kueleza masikitiko yao ni pamoja na Sonu Sood, Riteish Deshmukh na Parineeti Chopra.

Mkurugenzi Mkuu wa Kurugenzi ya Usafiri wa Anga, Faiz Ahmed Kidwai, ameliambia The Associated Press kwamba kulikuwa na abiria 232 na wafanyakazi 12 kwenye ndege hiyo, ambayo ilikuwa ikielekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick wa London.

Picha pia zinaonesha vifusi vikiwaka moto, huku moshi mzito mweusi ukipaa juu angani karibu na uwanja wa ndege.

Ajali hiyo ilitokea mara tu baada ya ndege kupaa, vituo vya televisheni viliripoti huku kituo kimoja kikionesha ndege hiyo ikipaa juu ya eneo la makazi na kisha kutoweka kwenye skrini kabla ya wingu kubwa la moto kupanda angani kutoka nje ya nyumba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button