Muigizaji India kufanyiwa upasuaji wa saratani ya ini leo

INDIA:MUIGIZAJI Shoaib Ibrahim ameandika ujumbe wa hisia kwenye wake wa Instagram, akieleza kuwa mkewe Dipika Kakar anatazamiwa kufanyiwa upasuaji wa saratani ya ini ambao utachukua muda mrefu.
Ibrahim amewaomba wadau wa filamu na wananchi kwa ujumla wamuweke katika maombi yao anafanyiwa upasuaji leo Juni 3, 2025.
Dipika amegundulika kuwa na saratani ya ini ya hatua ya pili ambayo ni nyakati ngumu mno kwake. Huku akidai leo ni siku kuu mno katika maisha yao kwa sababu ndiyo siku ya upasuaji huo.
Shoaib alitumia Hadithi za Instagram kuchapisha barua inayoshiriki kuhusu upasuaji wa mkewe. Hapo awali, upasuaji wake ulicheleweshwa kwa sababu ya maambukizo ya virusi na dalili kama za mafua.
“Upasuaji wa Dippi umepangwa kufanyika leo. Utakuwa ni upasuaji wa muda mrefu… anahitaji maombi na nguvu zako zote zaidi… tafadhali muweke katika maombi yako,” aliandika kwenye ujumbe huo.”
“Pamoja na familia yangu yote kuwa kando yangu na UPENDO wote na SALA zikimiminika kutoka kwenu nyote nitapitia hili pia! IshaAllah. Niwekeni katika maombi yenu! Upendo mwingi. Dipika,” alieleza Dipika.
Dipika amesema alikuwa akipata maumivu kutokana na jiwe kwenye kibofu cha mkojo. Dipika na Shoaib wana mtoto wa kiume Ruhaan.




