Stevo Simple Boy: Nawasiliana zaidi na Mama yangu

NAIROBI: MSANII wa Kenya Stevo Simple Boy ameweka wazi kuwa huwa anawasiliana zaidi na Mama yake kuliko watu wengine.
Hayo yamekuja baada ya kuulizwa katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Mipasho wakimtaka aweke wazi mtu anayewasiliana naye zaidi kwa simu naye hakusita alisema ni Mama yake.
“Huwa nawasiliana sana na Mama yangu kwa simu kuliko mtu mwengine yeyote,” amesema.
Pia katika mahojiano hayo pia walimuuliza tofauti na mawasiliano ya simu kwa kuzungumza naani huwa anawasiliana naye zaidia kwa ujumbe mfupi wa simu (SMS) pia alijibu kuwa ni Mama yake.
Majibu yake ya mara kwa mara yanakazia uhusiano wenye nguvu na mama yake mtu muhimu zaidi katika maisha yake ya kila siku.
Mahojiano hayo yaliendelea kuuliza zaidi emoji anayoitumia zaidi anapowasilia kwa sms na Mama yake huwa anaitumia alijibu kuwa ni;”Emoji ya moto.”