Bundesliga

Tah anasa Bayern bure!

MUNICH: MABINGWA wa Bundesliga Bayern Munich wamefanikiwa kumsajili kitasa cha kimataifa cha Ujerumani Jonathan Tah kwa uhamisho wa bure kutoka kwa mabingwa wa msimu uliopita Bayer Leverkusen baada ya mkataba wake kutamatika mwisho wa msimu wa 2024/25,

Tangazo la Bayern limesema kuwa Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamuweka jinini Munich hadi mwisho wa msimu wa 2028/2029, huku beki huyo akishindwa kuficha furaha yake ya kutua klabuni hapo akisema kilichomleta ni kutwaa makombe kama ilivyo ndoto ya kila mchezaji

“Nina furaha kubwa kuja Bayern, nataka kuyatimiza majukumu yangu hapa na nifanye kazi kwa bidi ili tufanikiwe kama timu na tushinde mataji mengi Pamoja” – taarifa ya Bayern imemnukuu Tah.

Tah alihudumu Leverkusen kwa miaka 10 huku akifanikiwa kutwaa taji la Bundesliga bila kupoteza mchezo (unbeaten) pamoja na DFB Pokal katika msimu wa 2023/24. Aliiambia Leverkusen kuwa hataongeza mkataba wake zaidi ya mwaka 2025 na aliagwa katika mchezo wake wa mwisho wa nyumbani mapema mwezi huu.

Bayern walihusishwa na kutaka kumsajili Tah katika dirisha la usajili la msimu wa joto wa 2024 huku akiwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, lakini The Bavarians waliikataa bei ya beki huyo kutoka Leverkusen na kuamua kusubiri mkataba huo utamatike.

Mahitaji ya beki wa kati ya Bayern yalianza baada ya beki wao wakati huo Eric Dier kuondoka na kujiunga na AS Monaco ya Ligue 1 mwishoni mwa msimu huu.

Related Articles

Back to top button